Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimsemai kuwa kipo tayari kumuongoza Rais John Magufuli katika kulinda rasilimali za Taifa ikiwemo madini.
Kauli hiyo imesemwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Vincent Mashinjiwakatia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Dkt. Mashinji amesema kuwa hatua anazochukua Rais Magufuli kuhusu Makinikia ziko kinyume na Ilani ya CCM ambapo katika ukurasa wake wa 26-28 haikuzungumzia kurekebisha sheria na mikataba ya madini, na kwamba ilani ya Chadema kwenye ukurasa wake wa 57-59 inaonyesha namna ya kuiongoza vizuri sekta ya madini.
Hata hivyo, Dkt. Mashinji ametaja hatua kadhaa ambazo amedai kuwa kama Rais Magufuli atazichukua, zitamuwezesha kushinda vita aliyoianzisha ikiwemo, kuleta katiba mpya, kurudisha ‘Bunge Live’ ili watanzania wawaone wabunge ambao ni mawakala wa uporaji rasilimali za nchi, ili wawahuku katika chaguzi zijazo.
“Kama anataka kulifanikisha hili kwa uwazi arudishe bunge live, arudishe mikutano ya hadhara sisi tusimame tuwaambie watanzia, tuwataje mafisadi wako wapi ili twende kupambana nao,” amesema.
Hatua nyingine alizotaja, ni kuzitoa hadharani ripoti zote mbili za makinikia, kuweka wazi mikataba ya siri iliyopitishwa na Bunge, kuwachukulia hatua waliohusika na upotevu wa rasilimali, pamoja na kuyafanyia kazi maoni ya wapinzani.