Aliyekuwa mwimbaji wa muziki wa Taarab Mzee Yusuph amesema kuwa ameacha muziki ile awe Muumuni wa Dini ya Kiislamu na kumfuata Mtume Muhammad (SAW).

Mzee Yusuph amesema hayo leo wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha Radio hapa nchini kuhusu kuacha kwake kwa muziki.

Baada ya kuacha muziki mwanamuziki huyo amesema kuwa baada ya kwenda kuhiji Makka na kushika Al Kaaba alimuomba Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu.

Mzee Yusuf amesema kuwa alipoanza kubadilika alikuwa anakataza pombe kwenye Band yake ya Jahazi Modern Taarab.

Mzee Yusuf amesema kuwa alipokuwa anakataza haya mambo wengi walikuwa wakimwambia kwa nini asifungue Madrasa.

Pia amesema kuwa alianza kubadilika kwa kuachana na starehe magoma kwanza maana ilikuwa ni kama kunywa maji tu unaposikia kiu wakati huo.

Mwisho alisema kuwa alimwambia kwanza mke wake mdogo kama ameacha muziki na kesho yake akamuambia mke wake mkubwa kama ameachana na mziki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *