Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki.
Waziri Kairuki amesema hayo leo bungeni mjini wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa waziri huyo.
Kairuki akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Iringa, Ritta Kabati aliyetaka kujua suala la ujazwaji wa nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wengi serikalini waliokumbwa na sakata la vyeti feki na kujiondoa wenyewe katika nafasi zao hizo kama ambavyo Rais Magufuli alivyoagiza.
Wakati akijibu swali hilo Waziri Kairuki alikiri wazi kuwa na upugufu wa watumishi jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa katika Taasisi mbalimbali za Umma na kuwahakikishia wananchi kuwa hayo yote yatakwisha hivi karibuni, kwani kibali cha ajira kimeshatolewa.