Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuacha matumizi ya mada ya kulevya.

Chid Benz ambaye aliwahi kushinda tuzo ya mwanahip hop bora amesema kwa sasa yupo fiti kiafya na kiakili na anachowaza ni muziki na maisha tu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumsaidia mpaka amefanikiwa kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kwamba hawezi kurudi nyuma wala kuthubutu kurudia kutumia dawa hizo za kulevya.

Chid aliendelea kuongeza kuwa tofauti na wakati wa nyuma alipokuwa anaishi mitaani kwenye mageto ya washikaji zake kwa sasa amerudi nyumbani kwao na anaishi na familia yake na maisha yametawaliwa na furaha.

Kuhusu muziki mwanamuziki huyo amesema kuwa ameshafanya nyimbo mpya na Q Chilla katika studio za Kill Records na anatarajia kutoa video mpya hivi karibuni.

Chid Benz kwa sasa yupo jijini Dar akitokea Zanzibar alikokuwa amekwenda mapumzikoni baada ya kutoka mkoani Iringa alikokuwa kwenye kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *