Beki wa klabu ya Liverpool, Mamadou Sakho ameendelea kuipaisha Tanzania kupitia mtandao wake wa Instagram kwa kuweka picha akiwa katika Mbuga ya Serengeti mkoani Mara.
Mchezaji huyo raia wa Ufaransa ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Crastal Palace msimu ulioisha yupo nchini kwa mapumziko na familia yake baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu nchini Uingereza.
Sakho amekuwa akiweka picha kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika kama yupo nchini kwa mapumziko na kutembelea mbuga za wanyama.
Beki huyo mtata ameongozana na mkwewe Majda pamoja na watoto wao wawili wa kike, Aida na Sienna ambao wanaoneka kufurahia safari hiyo.