Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema kuwa adhabu waliopewa ya kutohudhuria vikao vya bunge siyo silaha ya kuwafunga midomo.
Bulaya amefunguka hayo akiwa Mkoani Kilimanjaro na kusema kwamba uamuzi uliofanya na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge haijawatendea haki.
Bulaya amesema kuwa wananchi wao kwa sababu ni kwa muda mrefu watakosa wawakilishi bungeni ingawa siyo mwisho kwa wao kupigania haki na kuwatumikia wananchi kwa njia zingine.
Bulaya ametupa lawama kwa Ndugai na kudai kuwa ni kiongozi asiyeweza kuzuia hasira ndio maana amekuwa na maamuzi ya kuhukumu haraka wakati yeye ni baba anayepaswa kuwa na subira na uvumilivu wa kuongoza.
Esther Bulaya pamoja na Halima Mdee mbunge wa Kawe wamesimamishwa kuhudhuria vikao vyote vya Bunge vinavyoendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 kwa kile kinachodaiwa kuonyesha utomvu wa nidhamu ndani ya bunge.