Askari mgambo aliyetambulika kwa jina la Nurdin Kisinga amepigwa risasi jana mchana katika Kijiji cha Songa wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.

Tukio hilo la kinyama limetokea ikiwa saa chache baada ya IGP Simon Sirro kuzuru ukanda huo unaoongoza kwa mauaji ya raia yenye utata.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha mtu huyo kupigwa risasi na amesema majeruhi amelazwa Hospitali ya Songa, Mkuranga.

Kuhusu taarifa zinazosambaa kuwa mtu huyo amekufa, Kamanda Lyanga amesema anayeweza kuthibitisha kama amekufa au laa, ni daktari lakini taarifa alizonazo yeye ni kwamba amejeruhiwa kwa risasi.

Mtu mwingine, Eric Mwarabu ambaye alikuwa ni askari mgambo alipigwa risasi na kuuawa akiwa amejificha kwenye uvungu wa kitanda nyumbani kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *