Rais wa Marekani, Donald Trump ameunga mkono nchi ya Saudi Arabia kuitenga nchi ya Qatar.

Trump amesifu msimamo wa nchi hiyo ya tawala ya kifalme kwa kuitenga Qatar baada ya kutuhumiwa kusaidia kifedha makundi ya kigaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Tweeter, Trump amesema kwamba hatua hiyo inaweza kuwa ndio mwanzo wa kutokomeza tishio la ugaidi.

Kwa upande wake msemaji wa Ikulu Marekani, Sean Spicer, amesema mgogoro huo umekuwa ukifukuta kwa muda mrefu.

“kumekuwa na wasiwasi wa muda miongoni mwa nchi jirani na Qatar. Marekani inaendelea kuwasiliana kwa karibu na nchi zote ili kutatua mgogoro unaoendelea na kurudisha hali ya ushirikiano ambayo ni muhimu kwa usalama wa eneo”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *