Chama Cha ACT-Wazalendo kimemvua uenyekiti Anna Mghwira baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Maamuziki hayo yametangazwa leo na kaimu kiongozi wa chama hicho, Samson Mwigama baada ya kamati ya uongozi wa chama hicho kukutana na kuamua maamuzi hayo.
Mwigama amesema kuwa chama kimeamua kumvua uongozi huo kutokana na mgongano wa majukumu kati ya kazi yake ya mkuu wa mkoa na nafasi ya uenyekiti wa chama hicho.
Pia kaimu kiongozi huyo wa chama amemtaka Rais Magufuli kufanya majadiliano na viongozi wa vyama pinzani kama anataka kuteuwa watu ndani ya vyama hivyo.
Licha ya kufutwa uenyekti huo lakini mkuu wa mkoa huyo anaendelea kubakia mwanachama wa chama hicho kama alivyo Kitila Mkumbo ambaye alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Mwigama amesema kuwa chama kimemchagua Jeremia Maganja kuwa kaimu mwenyekiti mpaka uchaguzi mkuu wa chama utakapofanyika hapo baadae.