Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limetoa onyo kali kwa watu wanaoeneza taarifa  mitandaoni kuhusu kutangazwa kwa nafasi za ajira katika jeshi hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Utumishi wa jeshi hilo, Meja Jenerali Harrison Masebo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Meja Jenerali Masebo amebainisha hayo baada ya kuenea uvumi mitandaoni na mitaani kwa baadhi ya watu kujifanya wanahusika na jeshi hilo katika idara ya kutoa ajira kwa wananchi.

Pamoja na Hayo Meja Jenerali Masebo amesema mara zote Jeshi limekuwa likitoa ufafanuzi kuhusiana na masuala ya ajira lakini wanashangazwa na kundi hilo namna wanavyofanya kutaka kupitia ‘shortcut’.

Pamoja na hayo, Meja Jenerali Masebo aliendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema kuwa kila wao jeshi wanataratibu zao kwa kuchukua vijana kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi.

Meja Jenerali Masebo amewataka wananchi kuwaepuka watu hao wanaosambaza taarifa hizo kwani ni matapeli na hawausiani na jeshi la wananchi Tanzania hivyo wanatakiwa kuwaepuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *