Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard atakosa mechi za mwanzo wa msimu ujao wa Ligi kuu nchini Uingereza baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye kifungo cha mguu.
Hazard aliumia mfupa wa kifundo cha mguu wa kulia akifanya mazoezi akiwa an timu ya taifa ya Ubelgiji siku ya Jumapili.
Klabu yake Chelsea wamesema upasuaji huo aliofanyiwa jana ulienda vyema na kwamba anatarajiwa kukaa kwa miezi mitatu kabla ya kuanza kufanya mazoezi.
Hazard pia atakosa mechi za kabla ya msimu dhidi ya Arsenal, Bayern Munich na Inter Milan nchini Singapore mwezi Julai mwaka huu na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Arsenal mnamo tarehe 6 Agosti.
Hazard aliwasaidia sana Chelsea kushinda Ligi ya Premia msimu uliomalizika majuzi ambapo aliwafungia mabao 16 katika mechi 36.
Kupitia akaunti yake ya Twitter akiwa hospitalini na kiungo huyo ameandika “Kila kitu kilikwenda vyema kuhusu upasuaji wangu kifundo cha mguu, na saa naanza safari ya kuelekea kupata nafuu! Nitakuwa na nguvu zaidi. Asanteni kwa uungaji mkono wenu!!”.