Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana amemtaka mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuacha kuingiza siasa msibani.
Gwajima amesema kuwa mkuu wa mkoa huyo ambaye pia anakaimu ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro alitoa uamuzi wa kuzuia mwili wa aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo kutokuagwa katika uwanja wa Mashujaa.
Pia Gwajima amemshukia Mkuu wa Mkoa huyo kumzuia mbunge wa jimbo hilo Godbless Lema kutoongea katika msiba wa wanafunzi iliyotokea Karatu mkoani Arusha.
Gwajima amesema jambo lililofanywa na viongozi wa serikali kukataza Uwanja wa Mashujaa kutumika kuaga mwili wa Marehemu Ndesamburo siyo jambo la busara hata kidogo.
Amesema kuwa tetesi alizosikia kuwa alitoa maelekezo uwanja huo usitumike na badala yake vitumike Viwanja vya Majengo.