Baada ya kusambaa voice note inayosikika sauti ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiongea kimahaba na muigizaji, Wema Sepetu, mwenyekiti huyo ameikana sauti hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Sauti hiyo imeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii na kusababisha gumzo mjini kutokana na maongezi ya wawili hao.

Mbowe amesema kuwa analichukulia suala hilo kama taarifa za kawaida za maji taka zinazosambazwa kwa ajili ya kumchafua kwa itikadi za kisiasa.

Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai amesema kuwa taarifa hizo zinatengenezwa hazina ukweli wowote na kusisitiza sauti hiyo siyo ya kwake na si za kweli.

Mbowe amesema kuwa timu yake ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo limetengeneza kumchafua kwani kwasasa wapo kwenye msiba wa Philemon Ndesamburo mkoani Kilimanjaro.

Mbowe amesisitiza kuwa sauti hiyo siyo ya kwake kwani Wema ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni mwanachama wao na kwamba kama kuna mahusiano sio kweli ni taarifa za upotoshaji tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *