Baada ya askari walioagizwa kumtoa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika bungeni kuchelewa kufanya hivyo hatimaye askari hao wamepangiwa vituo vingine vya kazi.
Askari hao waliagizwa na Spika Ndugai kumtoa Mnyika Bungeni baada ya kukaidi kauli ya Spika ya kunyamaza na kukaa chini.
Spika Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo kutoka nje ya Bunge siku ya Ijumaa.
Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa mkoani Dodoma amesema kuwa askari hao wataendelea kuhamishwa mpaka pale watakapowapata wanaofaa.
Mnyika alitolewa bungeni Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa wabunge kusema ‘Mnyika mwizi’ akimhusisha na wizi wa madini.
Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua dhidi ya mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi.
Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayawezi kwenda hivyo. Baada ya majibizano kati yao Spika aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge