Kundi la Islamic State limethibitisha kuhusika na mlipuko wa London uliosababisha vifo vya watu saba na kujeruhi 21 siku ya Jumamosi.

Jeshi la polisi nchini Uingereza wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini London hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la Jumamosi ambapo watu saba waliuawa na wengine wapatao hamsini walijeruhiwa.

Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.

Kufuatia msako huo watu kumi na moja wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi mashariki mwa London.

Mwanamke mmoja raia wa Canada aliyeuawa katika shambulio la London ametajwa katika vyombo vya habari.

Taarifa ya familia yake imesema kuwa alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya wasio kuwa na makazi kabla ya kuhamia Ulaya kuishi na mchumba wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *