Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amememuagiza mkaguzi mkuu wa Serikali kuchunguza hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati na kituo cha afya cha mjini Gairo mkoani Morogoro.
Majaliwa ameyasema hayo wakati akihutubia wakazi wa mji wa Gairo na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Gairo ‘A’ ambapo amesema hajaridhishwa na maelezo ya mganga mkuu wa hospitali hiyo ya upatikanaji wa dawa.
Waziri mkuu amesema kuwa “Sasa ni lazima nilete mkaguzi kutoka ofisi yangu ili tupate picha halisi kama dawa zinazoletwa zinafika, na kama zinafika zinatumikaje. huyu mkaguzi atakuja kukukagua wewe mwenyewe na kwenye zahanati zako,”.
Pia amesema kuwa katika mkutano wake na watumishi Serikali amewaeleza kuwa wao ni maafisa wa kukaa ofisini tu na wala si kwenda sehemu yeyote kujua hali ikoje ya upatikanaji wa dawa.