Watu 6 wameuawa na wengine 48 wamejeruhiwa kwenye tukio la kigaidi lililotea jana jijini London nchini Uingereza.
Idara ya polisi imesema kuwa washambuliaji watatu kati yao wamepigwa risasi na polisi na kuuwawa baada ya kugundulika.
Hapo awali, visa viwili ambavyo vimesababisha kifo cha mtu mmoja na zaidi ya watu 20 kujeruhiwa vinachukuliwa kama vitendo vya kigaidi.
Ghasia zilianza baada ya gari moja kuingia ndani ya umati wa watembeaji miguu, katika daraja moja jijini London.
Tukio hilo ambalo linatukia majuma kadhaa tu baada ya watu 22 kuuliwa pale mhanga mmoja wa kujitolea kufa, alipojilipua ndani ya uwanja mmoja wa burudani huko mjini Manchester, limelaaniwa na viongozi mbalimbali duniani.