Kiongozi mkuu wa mbio za mwenge, Amour Hamadi amewataka wananchi na viongozi wote wilayani Kibiti kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuimarisha na kudumisha amani iliyopo.
Ameyasema hayo mara baada ya kukithiri kwa vitendo vya mauaji wilayani humo wakati wa kukimbiza mwenge ambapo amesema kuwa ni bora wananchi wakajikita katika kufanya kazi za maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.
“Amani ikidumishwa kila mmoja atatimiza majukumu yake ya kimaendeleo na kuongeza pato la taifa na la mtu mmoja mmoja, hivyo basi nawaasa wananchi wa wilaya ya Kibiti kuwa na ushirikiano ili kuweza kuondokana na tatizo hili,” amesema Hamad.
Hata hivyo ameongeza kuwa zipo nchi ambazo zilikuwa na machafuko makubwa ambayo yalisababisha nchi hizo kudidimia na kushuka kwa uchumi na ngazi ya taifa na mtu mmoja mmoja.