Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu maarufu kwa jina la Mzee Ngosha ambaye anayetajwa kuwa ni moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Misungwi Mwanza.

Mzee Francis Maige Kanyasu maarufu kwa jina la Mzee Ngosha alilazwa katika hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu ya kifua.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii) imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda kuzikwa huko.

Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa kesho Jumamosi saa 2 asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *