Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua kituo cha ukusanyaji kodi kwa njia ya Kieletroniki katika ofisi za TTCL Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema kuwa dirisha moja la ukusanyaji kodi kwa njia ya kieletroniki aliyozindua leo ni muarobaini kwa watu wanaokwepa kodi nchini.
Rais Magufuli amesema kuwa lengo la Serikali ni kukusanya mapato na kuwatambua wanaokwepa kodi kutokana kuna watu wengine hawapo tayari kulipa kodi.
Kwa upande mwingine Rais Magufulia amesema kuwa amefurahi kutembelea kituo cha ukusanyaji taarifa (Data Centre) na kusema kuwa umuhimu wake ni kukusanya na kulinda taarifa za nchi.
Rais Magufuli amesema kuwa amefurahishwa na mafanikio makubwa kwa nchi yetu pia amewashukuru waliowezesha mafanikio hayo.