Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema kuwa itaongeza nguvu zaidi katika vita ya kupambana na watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.

Kamishna huyo amesema kuwa itaongeza nguvu hizo ili kuokoa nguvu kazi ya Taifa ikiwa ni mkakati wa kutokomeza mtandao huo.

Rogers Sianga amesema kuwa lengo kubwa la serikali ni kutokomeza mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na biashara hiyo ili kuweza kuokoa kizazi cha sasa na kijacho.

Pia amesema kuwa toka Mamlaka hiyo imeanza wamefanikiwa kudhibiti uingizaji wa Heroine, Cocaine na dawa nyingine za kulevya na wamewakamata wafanyabiashara wakubwa ambao walikuwa wanatafutwa na mataifa makubwa.

Sianga ameongeza kuwa Serikali imepanga kuongeza vituo vya kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya katika Mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza kwa awamu ya kwanza kutokana na mafanikio yaliyofikiwa katika kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya na matumizi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *