Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa wanafunzi watatu wa Shule ya Luck Vicent wanaopatiwa matibabu nchini Marekani wanaendelea vizuri.

Nyalandu ameeleza kuwa hali za wanafunzi hao zinaendelea vizuri huku Sadia na Wilson wamepelekwa kwenye kituo maalumu kwa uangalizi wa karibu na Doreen ameendelea kuwepo katika wodi ya watoto Mercy Hospitalini.

Mbunge huyo ameeleza mtoto Sadia anaendelea vizuri pamoja na maeneo mengine ya mwili aliyoumia na kuvunjika.

Sadia alikuwa amevunjika shingo na kupitia maumivu makubwa ya wiki sita kabla ya shingo yake kurejea hali yake ya kawaida.

Kama ilivyoripotiwa hapo nyuma, Sadia na Wilson wamepelekwa kwenye kituo maalumu kwa uangalizi wa karibu, mjini Sioux City, katika Jimbo la Iowa, na wanaendelea vizuriI

Doreen ameendelea kuwepo katika wodi ya watoto Mercy Hospitalini, ameelezewa kuendelea kuimarika na mwili wake kuitikia matibabu anayoendelea nayo.

Doreen alifanyiwa upasuaji kwenye nyonga (Chini ya Kiuno), kwenye bega, kwenye kidevu, na mwisho kwenye uti wa mgonga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *