Mwanamuziki wa Marekani, Eminem ameguswa na tukio la ugaidi la Manchester nchini Uingereza ambalo liliuwa watu 22 na kujeruhi 60.

Eminem ameamua kuchangisha fedha ili kuchangia familia ambazo zimewapoteza ndugu zao kwenye tukio katika show ya Mwanamuziki wa Marekani, Arina Grande.

Rapa huyo ametumia mtandao wake wa Twitter wenye wafuasi zaidi ya milioni 20 kuwahamasisha watu kuchangia fedha ili kufanikisha lengo lake.

Pia ameongeza kwa kuandika “Tafadhali niunge mkono katika kuwasaidia waathirika wa Manchester na familia zao, kwa kuchangia kupitia @BritishRedCross na @MENnewsdesk,”.

Eminem pia aliwaelekeza wafuasi wake kwenye ukurasa wa ‘JustGiving’ ambao alijiunga nao hivi karibuni kwa lengo la kuchangia waathirika, alipotoa tangazo kuwa atarudi jijini Manchester kufanya tamasha lenye faida kwa waathirika.

Hadi sasa ukurasa huo umeshachangisha zaidi ya $2.2 million kwa ajili ya waathirika wa tukio hilo lililotokea jijini Manchester nchini Uingereza.

Katika hatua nyingine, Eminem amewaonjesha mashabiki wake mpango wa kuwapa kitu kipya kwenye tamasha lake la kumbukumbu ya miaka 15 ya albam yake ya tatu ‘The Eminem Show.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *