Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) kupitia wakili wake, Hashimu Mziray imewasilisha ombi la kukata rufaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Rufaa hiyo ni kupinga uamuzi uliotolewa Mei 21, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa kuyatupilia mbali maombi yao waliyoyafungua mahakamani hapo dhidi ya wabunge wawili, Magdalena Sakaya(Kaliua),  Maftah Nachuma(Mtwara Mjini) na wenzao sita.

Walikuwa wakiomba mahakama hiyo iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya uongozi na kufanya mikutano ya chama.

Akiwasilisha kusudia la kukata rufaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mziray alisema hawakuridhika na uamuzi huo kwa sababu si kweli kuwa  CUF haina bodi ya wadhamini.

Wakili Mziray alisema CUF ni chama ambacho kipo hai, kina wabunge, madiwani, majengo, wanachama na hata Msajili wa Vyama vya Siasa hajakifuta.

Alibainisha kuwa Hakimu Mashauri akulielewa tangazo la Wakala wa Vizazi na Vifo(RITA) hivyo wanaiomba Mahakama Kuu kutengua uamuzi wake kwa madai kuwa ni batili.

Awali katika uamuzi uliotolewa na Hakimu Mashauri ambao uliyatupilia mbali maombi ya Bodi hiyo alizisikiliza pande zote mbili na kuzitolewa uamuzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *