Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha mkuu mpya wa jeshi la Polisi nchini, IGP, Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amechukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa Jeshi, Ernest Mangu ambaye uteuzi wake umetenguliwa jana na Rais Magufuli.
Sirro baada ya kuapishwa amekula kiapo cha maadili mbele ya Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mapya.
Sherehe za kuapishwa kwa kamanda huyo mpya wa jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro zimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vingozi mbali mbali wa Serikali pamoja na maofisa wa Polisi.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria kwenye sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Kwa mujibu ya Taarifa hiyo iliyopitolewa jana ilimesema kuwa Ernest Mangu atapangiwa kazi nyingine ya kufanya.