Nchi ya Japan imeishutumu vikali Korea Kaskazini kuhusu majaribio ya silaha za nyuklia ambayo imekuwa ikiendelea kuyafanya katika bahari ya Japan kwaajili ya kulinda usalama wake dhidi ya maadui zake.
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema kuwa kitendo hicho si cha kawaida na kwamba kinatishia usalama wa mataifa jirani na dunia kwa ujumla ambapo hata katika mkutano wa G 7 majaribio hayo yamejadiliwa kiundani zaidi.
Waziri Abe amesema kuwa majaribio hayo ya makombora ya Korea Kaskazini yanahatarisha shughuli za uchukuzi ndani ya Bahari nchini Japan ambapo shughuli mbalimbali zimekuwa zikisimama kwa kuhofia usalama..
Hata hivyo, Korea Kaskazini imekuwa na choko choko dhidi ya Marekani kuhusiana na mpango wake wa nyuklia na hatimaye Japan nayo imeguswa na harakati hizo za Korea Kaskazini.