Muigizaji nyota wa Markani, Dwayne ‘The Rock’ Johnson ametangaza kuwa atawania urais wa Marekani mwaka 2020 wakati akitumbuiza mashabiki wake katika kipindi maarufu cha Saturday Night Live.

Mwigizaji maarufu Tom Hanks alikubali kuwa naibu rais kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 20120.

Baadaye, mwigizaji huyo anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ulimwenguni alisema tangazo hilo lilikuwa la utani.

Hata hivyo alisisitiza kwamba Marekani inahitaji viongozi walio na uwezo wa kuongoza, wanaojali maslahi ya taifa hili na raia wake.

Mbali na muigizaji huyo kutaka kugombea urais, mwanamuziki wa Marekani, Kanye West naye ni miongoni mwa wasanii wanaoutamani urais wa Taifa hilo kubwa ulimwenguni.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *