Beki wa kati wa Arsenal, Per Mertesacker atakosa mechi za kwanza za ufunguzi wa ligi kuu nchini Uingereza msimu ujao baada ya kuumia goti wiki iliyopita.

Kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger amesema kwamba beki huyo atakuwa nje kwa miezi michache baada ya kuumia goti kwenye mechi ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Lens siku ya Ijumaa ambapo walitoka sare.

Mertesacker mwenye umri wa miaka 31, akusafiri na kikosi hicho kilichoenda nchini Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza.

Wenger ameshamsajili Rob Holding kutoka Bolton ambaye ni beki atakayeziba pengo hilo akishirikiana na Laurent Koscielny  Gabriel Paulista katika beki ya kati.

Mertesacker alijiunga na klabu hiyo mwaka 2011, ambapo amecheza mechi 24 kwenye ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita.

Akiwa uwanjani akiitumikia timu yake kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.
Mertesacker: Akiwa uwanjani akiitumikia timu yake kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *