Watoto wawili majeruhi wa ajali ya gari la Shule ya Lucky Vincent ambao wanatibiwa nchini Marekani wameruhusiwa kutoka hopitalini.
Taarifa hiyo imetolewa na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Watoto hao walioruhusiwa kutoka hospitali ni Sadia Ismael na Wilson Tarimo waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mercy ya Marekani na sasa wapo katika makazi mapya.
Nyarandu ameanidka kama ifuatavyo “Watoto Sadia na Wilson waruhusiwa rasmi kutoka hospitali ya Mercy na wanaelekea kwenye makazi yao mapya mjini Sioux City IA”.
Pia ameongeza kwa kuandika “Mungu azidi kuwaangazia nuru ya uso wake. Amani iwe nawe na Nesi wetu mpendwa kwa huduma kubwa mmefanya kwa watoto hawa na Tanzania,”.
Lakini mwanafunzi Doreen ataendelea kuwepo hospitali katika wodi ya watoto akiendelea kupata huduma za karibu hadi itakapoamuliwa hapo baadae.