Kesi inayomkabili Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi imeshindwa kuendelea kusikilizwa kwa mara ya nne mfululizo baada ya wakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani.

Hayo yamesemwa mahakamani hapo na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga ambapo amesema kuwa alipewa taarifa na wakili wa Scorpion kuwa alikuwa na kesi nyingine Mahakama kuu hivyo hatoweza kuhudhuria mahakamani hapo.

Wakili Katunga amesema kuwa “Mheshimiwa hakimu, mshtakiwa yupo mbele ya mahakama yako lakini nimepata taarifa kutoka kwa wakili wake kuwa yupo Mahakama Kuu kwa Jaji Wambura mbapo anasikiliza kesi.

Ameendelea kwa kusema hivyo tunaiomba Mahakama yako itoe ahirisho la mwisho na kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi,” amesema Katuga.

Kwa upande wa Hakimu Mkazi, Flora Haule anayesikiliza shauri hilo amekubalia ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 8, mwaka huu na mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *