Kampuni ya SportPesa imeandaa mashindano maalumu ya soka yatakayo julikana kama SportPesa Super Cup mashindano hayo yanatarajia kushirikisha timu za Tanzania, Zanzibar na Kenya ambazo zinadhaminiwa na kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari kwamba, Bingwa wa michuano hiyo atapata dola za Kimarekani 30,000 na nafasi ya kucheza dhidi ya timu ya England.
Amezitaja timu hizo kuwa Simba SC, Yanga SC na Singida United kwa Tanzania Bara, Jang’ombe Boys ya Zanzibar, Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC za Kenya.
Tarimba amesema kwamba michuano hiyo itaanza Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11 na itafanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
RATIBA YA SPORTPESA SUPER CUP
Juni 5, 2017
Singida United Vs FC Leopard
Yanga SC Vs Tusker FC
Juni 6, 2017
Jang`ombe Boys vs Gor Mahia
Simba Vs Nakuru All Star
NUSU FAINALI
Juni 8, 2017
Singida United/AFC Leopards Vs Yanga SC/Tusker FC
Simba SC/Nakuru All Star Vs Jangombe Boys/Gor Mahia
FAINALI
Juni 11, 2017