Polisi watatu wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio lililotea leo asubuhi katika eneo la Liboi kaskazini mashariki mwa Kenya karibu.

Duru za usalama zinaarifu kuwa gari la kijeshi lililokuwa limewabeba maafisa wa usalama wa Kenya lilikanyaga bomu la kutegwa ardhini.

Taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari Kenya zinasema kuwa maafisa hao walikuwa wanapiga doria katika eneo la Kulan wakati gari lao lilipokanyaga mlipuko huo.

Maafisa wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo na inaarifiwa wamesafirishwa hadi mjini Nairobi kupata matibabu maalum.

Gazeti la Daily Nation linaripoti kuwa maafisa hao walikuwa wanasafiri kwa gari la kituo cha polisi cha Kulan katika barabara ya Liboi – Milan wakati gari hilo lilipokanyaga bomu la kutegwa ardhini.

Makamu wa rais William Ruto ametuma ujumbe katika Twitter akisema, “Waathiriwa wa shambulio la Liboi kaunti ya Garissa wamo mawazoni mwangu. Ni lazima tuujenga ukuta mpakani”.

Serikali ya Kenya iliidhinisha ujenzi wa ukuta katika mpaka baina ya Kenya na Somalia kuzuia uhalifu baada ya shambulio la kigaidi dhidi ya chuo kikuu cha Garissa mnamo mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *