Serikali imesema kuwa kuna baadhi ya Magereza nchini zinashindwa kutekelezeka baadhi ya haki za wafungwa kutokana na msongamano.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ambapo amesema serikali itajenga magereza katika maeneo yenye shughuli za Kilimo ili Shughuli ya kurekebisha tabia iendane na Uzalishaji.

Mwigulu amesema kuwa kutokana na hayo Serikali imeweka mkakati maalum ambao utasaidia kuondoa changamoto hiyo kwa jeshi la Magereza nchini.

Mwigulu amesema kuwa mkakati huo ni pamoja na kuwahamisha Wafungwa ambao wameshahukumiwa katika magereza ya mijini na kuwahamishia maeneo yatakapojengwa magereza kwa ajili ya kwenda kutumikia vifungo huku wakiendelea na shughuli nyingine za Ujenzi wa taifa.

Katika hatua nyingine amewataka maafisa Masuhuri kuelekeza fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipia huduma mbalimbali ikiwemo Umeme katika taasisi za kiserikali ili kuepuka changamoto zitakazoweza kujitokeza pindi huduma hizo zitakapositishwa kutokana na kutokulipa kwa wakati.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *