Nyota wa tenisi kutoka Urusi Maria Sharapova, amenyimwa kadi maalumu ya kuingia kwenye mashindano ya French Open yatakayoanza baadae mwezi huu.

Mkuu wa chama cha tenisi nchini Ufaransa Giudicelli Ferrandini mwaliko huo ungeliweza kutolewa kwa mchezaji ambaye ametoka kuwa majeruhi lakini sio kwa aliyefungiwa kwa kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Sharapova, mshindi mara tano wa Grand Slam, alimaliza kifungo cha miezi 15 hivi karibuni na hakuwa na alama za kutosha za kuingia katika droo kubwa ya kushiriki michuano hiyo.

Sababu ya kukataliwa kuingia kwenye mashindano hayo inatokana na kashfa yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli michezoni.

Mashindano ya French Open yanatajia kuhirikisha wachezaji tenisi kutoka mahali mbali mbali ambayo yanatarajia kuanza mapema mwezi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *