Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa polisi aliyemtishia bunduki aliyekuwa naibu waziri wa fedha, Adam Malima alikuwa sahihi.

Sirro amesema kuwa askari huyo amefyatua risasi hewani ili kuwatia nguvuni watuhumiwa ambapo walikuwa wanakaidi agizo la askari.

Kamanda Sirro amesema hayo leo pindi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kuenea maneno sehemu mbalimbali zikidai polisi hao hawakutumia busara katika kufanya kazi yao.

 “Kimsingi ninachosema ile bunduki  tunayowapa askari ni kwaajili ya matumizi na tumewapa maelekezo..Kikubwa wananchi wajue suala la utii wa sheria bila ya shuruti ni la msingi’.

 Pia amesema kuwa ‘kama ukikataa kutii sheria tuna kila namna tunahakikisha tunakukamata na kukupeleka panapo husika’.

 Ameongeza kwa kusema kuwa “Kwa hiyo askari Polisi alichokifanya ni kutumia uzoefu wake, umakini wake kuhakikisha kwamba gari ambalo ni kielelezo, dereva ambaye ni mtuhumiwa na Mhe. Malima ambaye ni mtuhumiwa wanapelekwa vituo vya polisi na wamefanikisha hicho na leo amepelekwa mahakamani”.

Katika hatua nyingine, Malima ameachiwa huru kwa dhamana ya Milioni tano baada ya jana kuweka kizuizini na leo kupandishwa Mahakamani kwa kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *