Aliyekuwa naibu waziri wa fedha wa awamu ya nne, Adam Malima leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kuwazuia polisi kufanya kazi yao.

Mlalamikaji katika kesi hiyo ni askari H.7818 PC Abdul akiwa kazini na maafisa wa Kampuni ya PBEL inayojihusisha na kukamata watu wanaopaki magari hovyo ambapo tukio hilo lilitokea jana eneo la Double Tree Hotel Masaki.

Mlalamikaji amedai alizuiliwa kutekeleza wajibu wake na waziri mstaafu huyo huku akishirikiana na wanachi kuwazuia askari hao ambapo askari huyo aliamua kupiga risasi sita hewani ili kuwatuliza watu waliokuwa wanazomea wakiongozwa na mtuhumiwa.

Mtuhumiwa pamoja na dereva wake walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Oysterbay jana na kufunguliwa kesi yenye namba OB/RB/7306/2017.

Aidha mahakama imemwachilia huru Malima kwa dhamana ya shilingi milioni tano na kesi yake itaendelea hapo baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *