Rais wa shirikisho la soka duniani “FIFA”, Gianni Infantino amesema ataiongezea Bara la Afrika nafasi ya timu mbili kwenye mashindano ya kombe la dunia kama zitaongezeka na kufikia 40 mwaka 2026.

Infantino alikuwa na mpango wa kuongeza timu kutoka 32 kwasasa mpaka kufikia 40 kabla ajachaguliwa kuwa rais wa shirikisho hilo mwezi Februari mwaka huu.

Kwasasa Bara la Afrika lina nafasi ya kuingiza timu tano kwenye mashindano ya kombe la dunia kwa hiyo kama rais huyo akiongeza timu mbili itafikia idadi ya timu saba.

Mpango huo wa kuongeza timu na kufikia 40 utaanza kwenye mashindano ya kombe la dunia mwaka 2026 kwasababu timu 32 zishathibitishwa kwenye mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi na mwaka 2022 nchini Qatar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *