Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Neddy Music amewataka wasanii kutoka Zanzibar wajitume na kuacha kulalamika.
Msanii huyo amesema hayo baada ya wasanii wa Zanzibar kusema kuwa kukosa usimamizi ndiyo chanzo cha kushindwa kufanya muziki wa Bongo Fleva.
Nedy amesema kuwa siyo kwamba wadau wa muziki wa Zanzibar wameshindwa kuwekeza lakini wanaogopa kutoa pesa pasipo kuwa na uhakika kama mahali anapowekeza patamletea manufaa kwake.
Nedy amesema kuwa siyo kwamba Zanzibar hakuna wadau wakuendeleza muziki lakini wasanii je waliopo wameweza kuonyesha kitu walichonacho ili kuwa prove wrong wadau.
Pia amesema kuwa Unatakiwa kumshawishi mdau wa muziki akuone wewe ni dhahabu na akiweka pesa yake ajue haiwezi kupotea.
Ameongeza kwa kusema kuwa Mara nyingi nikipata nafasi huwa nawashauri waweze kujionyesha uwezo wao na siyo kulalamika. Wewe usipojitangaza hakuna atakayeota kuwa wewe unathamani katika muziki na mimi ndipo nilipotokea kufanya kazi bila kukata tamaa.
Hata hivyo Nedy amefunguka na kusema kwamba suala la dini lisiwe kikwazo kwani muziki nao ni sehemu ya ajira hivyo kinachotakiwa ni wao wenyewe kutenga muda wa kazi na na muda wa kufanya ibada.