Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘MO’ ameiandikia barua Simba akiitaka wamlipe fedha zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji tangu mwaka jana kiasi cha shilingi bilioni 1.4.

Hayo yamejiri siku moja baada ya Simba kutiliana saini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa.

Uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa timu, Evans Aveva, ulisaini mkataba huo wa miaka mitano na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.

MO amewaandikia Simba ‘demand note’ kwa kuwa wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe fedha kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.

Klabu hiyo ya Simba imeanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *