Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amesema amesekitishwa na hatua ya Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kuzuia kongamano la Demokrasia lililotarajiwa kufanyika leo.

Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya nne amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa ameshangazwa na kitendo hiko kwa kuwa kongamano hilo lilikuwa na nia ya kujadili mambo mbali mbali kwa mustakabali wa Taifa.

Lowassa amesema kuwa serikali imezuia mikutano ya hadhara wametii na sasa wameamua kufanya mikutano ya ndani bado inawafatilia.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari Lowassa aliambatana na mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya kongamano hilo, Makongoro Mahanga.

Kongamano hilo lilitakiwa kufanya katika ukumbi wa Anatouglou jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *