Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemfukuza kazi mkuu wa Jeshi la nchi hiyo Jenerali Paul Malong.
Jenerali Malong anaonekana na raia wa Sudan wengi kama mtu mwenye nguvu, na wanasubiri kuona atakavyopokea kuondolewa katika nafasi hiyo.
Hata hivyo mpaka sasa hakuna chombo chochote cha serikali nchini Sudan Kusini kilichotoa sababu ya kufukuzwa kiongozi huyo.
Katika siku za hivi karibuni maafisa wengi wa ngazi za juu wamekuwa wakijiuzulu na pia wengine kutoka serikali ya Sudan Kusini.
Wengi wamekuwa na wasiwasi kuhusiana na upendeleo wa kikabila na uhalifu wa kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo yameiingiza Sudan kusini katika mgogoro uliodumu kwa miaka minne sasa.