Mwanafunzi mmoja nchini Iran, Reza Parastesh amezua gumzo nchini humo baada ya kufanana na Lionel Messi.

Watu wengi katika mji wa Hamaden wamekuwa wakiomba kupiga picha na kijana huyo aitwaye Reza Parastesh na hivyo kusababisha msongamano wa watu kila atakakokanyaga, hivyo polisi walilazimika kumhifadhi kwa muda ili kuondoa msongamano huo.

Mkanganyiko huo ulianza miezi michache iliyopita wakati baba wa kijana huyo aliyefanana mno na Messi alipompiga picha akiwa amevalia fulana ya timu ya Barcelona yenye namba kumi.

Reza Parastesh ana umri wa miaka ishirini na mitanohivi karibuni alianzisha mtindo wa ukataji nywele na kupunguza ndevu zake mithili ya mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina.Parastesh akiwa katika picha na mabibi waliotaka ridhaa yake

reza-parastesh-a-doppelganger-of-barcel

Reza Parastesh, kwa sasa amebatizwa jina ‘Messi wa Iran’ amejikuta kila wakati na kila mahali akiombwa kupiga picha na watu wa aina kwa aina katika mji wa nyumbani kwao Hameden, nchini Iran.

Kijana huyo amesema kwamba kwa sasa watu watu wananiona mimi kuwa ndiye Messi wa Iran na kunitaka nifanye kiila kitu afanyacho Messi halisi, na pindi ninapotokeza mahali, watu hupatwa na mshtuko.

Nina furaha kubwa kuona kwamba ninawapa furaha na hili linapotokea linanipa ari mpya kwa wananchi kutokana na kufanana na Messi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *