Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) imesema kuwa hali ya vipindi vifupi vya mvua katika mwambao wa Pwani ya Kaskazini itaendelea hadi kesho Mei 9 mwaka huu.
Taarifa ya tahadhari iliyotolewa na Mamlaka hiyo imesema kunatarajia kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.
Mamlaka hiyo imesema kuwa maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba.
TMA wamesema kuwa hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini.
Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo tajwa wanashauriwa kuchukua hatua stahiki kutokana na mvua hizo.