Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephath Gwajima amemtaka Spika wa Bunge kuahirisha kikao cha Bunge siku ya kuaga miili ya watoto waliofariki kwa ajali ya jana.
Amesema kama Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliamuru viongozi kusimama kwa kuwakumbuka watoto hao itakuwa ajabu kwa bunge kuendelea na vikao vya Bunge
Amesema Spika akiahirisha Bunge kwa siku moja itatoa nafasi kwa wabunge hao kwenda Arusha ili kuomboleza pamoja.
Meya wa Jiji la Arusha , Mh. Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu.
Miili hiy ya wanafunzi kesho inatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Lazaro amesema kuwa viongozi mbali mbali wakiwemo mawaziri pamoja na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vicent kwa ajili ya kikao na baadae majira ya saa tisa au kumi taarifa rasmi ya serikali itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha