Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alikuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Kauli hiyo ya Polepole imnafuatia baada ya kutoonekana hadharani katibu mkuu huyo kwa kipindi kirefu toka kumalizika kwa mkutano mkuu wa CCM mkoani Dodoma.

Polepole amesema kuwa Kinana alikuwa akiugulia afya yake pindi yupo kazini hivyo alichukua muda wa kutosha kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu kutokana na Afya yake kuteteleka.

Katibu mkuu huyo wa Itikati  amesema wakati Kinana akiwa hata kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya.

Pia amesema“Tangu akiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya, alikuwa anafanya yote haya akiugulia afya yake kwahiyo ikakubalika achukue muda wakutosha wa kuitizama afya yake nje ya nchi na anapo rejea mgonjwa akitoka hospitali huwa hakimbii kazini.

Abdulrahman Kinana hajaonekana hadharani kwa muda tangu Rais Magufuli aliposema kuwa yuko India kwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *