Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mabeste amesema kuwa hajawahi kuwa na urafiki na wasanii wenzake kwa kuwa hapati mawazo mapya kutoka kwa wasanii hao.
Mabeste amefunguka hayo kwa kusema kuwa wasanii wengi anaonekana nao wanakutana kikazi na siyo kirafiki kwani hawampi mawazo mapya ya kumfanya ajiongeze katika kazi zake.
Mkali huyo wa ‘Baadae Sana’ amesema kwamba tofauti na mke wake marafiki zake wengine ni watu waliopo nje ya muziki kwa kuwa wao ndio wanaona kipi kinafanyika katika tasnia na ndio washauri wa kumuelekeza kipi cha kufanya na kipi cha kuacha
Mabesster amesema kuwa “Ukiacha kuwa kwa wasanii kuna unafki mimi mke wangu ndiyo rafiki yangu.
Pia ameendelea kusema kuwa huwezi kunikuta katika sehemu za starehe kwa sababu sina hao marafiki wa kutoka nao.
Mabeste ameendelea kusema kuwa Unajua mkiwa uwanjani hamuoni mnayoyafanya, ila waliopo nje ndo wanajua.
Mwisho amemaliza kusema hata nikisema wasanii wenzangu ndio wa kushauriana nao basi itafika sehemu mawazo yatafika ukomo kwa sababu tunawaza wote sawa.