Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo amewasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma.
Katika uwasilishaji wa bajeti hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa malaria imeendelea kuwa changamoto nchini licha ya kugawa vyandarua na kupulizia dawa katika mikoa mbalimbali nchini.
Pia waziri Ummy amewataka wenye dalili za kifua kikuu wajitokeze kwa kuwa kinatibika.
Pia amesema hudumu za kusafisha damu na figo zimeanza kupatikana katika hospitali za kanda.
Waziri huyo hakusita kuzilaani halmashauri zote ambazo hazikutoa fedha za mfuko wa maendeleo ya wamawake.
Kuhusu mauaji ya wazee, Waziri Ummy amesema yamepungua kutoka 190 mwaka 2015 hadi 134 mwaka 2016.
Waziri Ummy ametaja vipaumbele vya wizara yake ambavyo ni kuimarisha kinga na tiba, huduma za mama na watoto, upatijanaji wa dawa, kuimarisha vituo vya afya na hospitali, kuimarisha huduma lishe, matumizi ya tehama na kuongeza wanaotumia bima ya afya.
Ameeleza hakuna mjamzito atakayefariki kwa kukosa dawa ya kuzuia kifafa cha mimba na amesema zimetengwa Sh 7 bilioni kwa ajili yake.