Baada ya mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kufunga magoli matatu kwenye nusu fainali ya klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid ameweka rekodi rekodi muhimu tano.

Ronaldo amefikisha mabao 103 kwenye michuano hiyo ambapo ni mabao matatu zaidi ya timu nzima ya Atletico Madrid ambayo imefungaa mabao 100 pekee katika historia ya ushiriki wake kwenye michuano hiyo.

Pili mabao hayo matatu yamemfanya Ronaldo awe amefunga hat-trick saba kwenye historia ya michuano hiyo na kumfikia Lionel Messi wa Barcelona aliyefikisha idadi hiyo miezi michache iliyopita.

Pia Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 20 katika mchezo wa wapinzani wa jadi wa jiji la Madrid yaani Madrid dabi.

Mabao hayo matatu pia yamemfanya Ronaldo awe mchezaji wa kwanza kufunga hat-tricks (mabao matatu) zimazofuatana ( back-to-back) katika hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya. Ikumbukwe katika hatua ya robo fainali Ronaldo alifunga hat-trick dhidi ya Bayern Munich.

Mwisho mabao hayo matatu yamemfanya Ronaldo afikishe mabao 13 kwenye michezo ya hatua ya nusu fainali na kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye hatua hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *