Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini ndiye chanzo cha mgogoro ndani ya chama hicho kwa maslahi yake binafsi.

Maalim Seif amesema hayo leo wakati wa mahjiano na kituo kimoja cha runinga nchini baada ya kuulizwa nini chanzo cha mgogoro wa CUF.

Katibu mkuu huyo amesema kuwa hakuna haja ya wanachama kuwa na hofu kuwa chama hicho kinaweza kusambaratika hivyo amewataka kuimarisha mshikamano uliopo ndani ya chama hicho.

Pia amesema kuwa CUF haina mgogoro kama inavyoelezwa na baadhi ya watu, isipokuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini anajaribu kupandikiza mgogoro huo kwa maslahi yake binafsi.

Maalim Seif ameongeza kwa kusema kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanatumiwa kutaka kukivuruga chama hicho hivyo amesema kamwe hawatafanikiwa.

Mwisho amesema yeye kama kiongozi ataendelea kufanya shughuli zake za chama na kuwataka walio chini yake wasivunjike moyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *