Mwanamuziki wa nyimbo za asili nchini, Mrisho Mpoto amewafungukia watu wanaomtukana pamoja na kumtupia maneno ya kejeli baada ya kuonyesha nia ya kumuunga mkono Rais Magufuli.
Hayo yamejiri baada ya baadhi ya watu kumkejeri mwanamuziki huyo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuiunga mkono Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli.
Kupitia akaunti yake ya Instagram mwanamuziki huyo ameamua kuvunja ukimya baada ya kuwapasha ukweli watu hao wasiokuwa na mema kwake kutokana na kumgombanisha na Rais Magufuli.
Mpotoa ameandika kama ifuatavyo.“Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna “KUKUBALIANA KWA KUTOKUBALINA” lakini kumtukana mtu mwingine sio busara hata kidogo, kwa kuwa tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia,”.
Pia ameongeza “Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni yakuwa nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI jana, naomba niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa nilioyasema. Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo,” ameongeza.
Mwisho amemaliza kwa kusema “Kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa Rais kunaibuka kundi la wapinga maendeleo na kuanza kutukana. Naomba ijulikane kuwa sababu za kumunga mkono Rais, yale niliyokua nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!! MRISHO MPOTO mpaka sasa namuunga mkono Rais MAGUFULI. Iwe nachumia tumbo kama inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe,’.
Mpoto amesema kuwa yeye ataendelea kumuunga mkono Rais huyo kwa kuwa ni kiongozi ambaye anawapigania wananchi wa chini.